• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wafugaji mkoani Kilimanjaro walilia soko la maziwa

    (GMT+08:00) 2019-01-23 19:50:28

    Kuzorota kwa soko la maziwa ya mifugo wa kisasa katika Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, kunaweza kuvunja moyo kwa wafugaji maeneo mbalimbali nchini.

    Hayo yalielezwa na Mratibu wa Shirika la Maendeleo la Uholanzi (SNV), Isack Kitururu, wakati wa mafunzo ya namna bora ya uandaaji wa mpango mkakati wa uboreshaji wa masoko hasa katika uongezaji wa thamani.

    Mafunzo hayo yaliandaliwa na Jukwaa la Masoko na Mawasiliano la ABC BROS, kwa ushirikiano na SNV.

    Kwa mujibu wa Kitururu, Mkoa wa Kilimanjaro, soko la maziwa lipo na kinachotakiwa ni kuweka mikakati kuandaa bidhaa bora kabla ya kumfikia mlaji.

    Akifungua warsha hiyo, Ofisa Mifugo na Uvuvi wa Wilaya hiyo, Elia Machange, kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo, alisema mpaka sasa wana uwezo wa kuzalisha lita milioni 36 kwa mwaka, licha ya kuwa bado wana viwanda viwili vya usindikaji wa maziwa yao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako