• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya kutumia simu za mkononi kufanya sensa ya mwaka 2019

    (GMT+08:00) 2019-01-24 08:55:30

    Kenya inapanga kutumia simu za mkononi za kisasa kufanya sensa ya watu na nyumba ya mwaka 2019.

    Akiongea na wanahabari jana mjini Nairobi, Waziri wa fedha wa Kenya Bw. Henry Rotich amesema serikali inapanga kutumia zana za mkononi laki 1.65 kwa ajili ya sensa ya taifa itakayoanza mwezi Agosti.

    Bw. Rotich amesema matumizi ya zana za mkononi yataimarisha ubora wa data kwa kuwa zina uwezo wa kujikagua zenyewe data zilizokusanyika na kusahihisha zile zilizokosewa.

    Waziri huyo amesema Kenya inataka kuiga mfano wa nchi nyingine za Afrika zikiwemo Misri, Senegal na Ethiopia, ambazo zimefanya sensa za taifa bila kutumia karatasi. Ameongeza kuwa sensa iliyopita iliyofanyika mwaka 2009, ilionesha kuwa Kenya ilikuwa na watu karibu milioni 39.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako