• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wakandarasi wa China watajwa kutoa mchango chanya kwenye soko la nyumba Kenya

    (GMT+08:00) 2019-01-24 08:55:51

    Wakandarasi wa China wametajwa kutoa mchango chanya kwenye soko la nyumba nchini Kenya. Mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya maendeleo na usimamizi wa ardhi ya Kenya Bw. Mwenda Makathimo ameliambia shirika la habari la China Xinhua mjini Nairobi kuwa, wakandarasi wa China wameboresha ufanisi wa ujenzi kwenye sekta ya nyumba nchini humo.

    Akiongea kwenye uzinduzi wa ripoti kuhusu hali ya utoaji huduma kwenye sekta ya nyumba, Bw. Makathimo amesema wakandarasi wa China wameongeza ugavi wa nyumba za bei nafuu, na hivyo kusaidia kutuliza bei ya nyumba nchini humo.

    Bw. Makathimo amesema wakandarasi wa China wameleta nidhamu na ufanisi kwenye sekta ya ujenzi ya Kenya, na wakandarasi wa Kenya wana mengi ya kujifunza kutoka kwa wenzao wa China, hasa kuingiza teknolojia mpya kutoka China kwenye sekta ya nyumba ya Kenya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako