• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yatajwa kuwa na hatari ya chini ya kiusalama licha ya shambulizi la kigaidi la wiki iliyopita

    (GMT+08:00) 2019-01-24 08:56:13

    Kenya imetajwa kudumisha kiwango cha chini cha hatari ya kiusalama licha ya shambulizi la kigaidi lililotokea wiki iliyopita mjini Nairobi na kusababisha vifo vya watu 21.

    Mkurugenzi wa mauzo kanda ya Ulaya na Afrika, Kampuni ya ushauri kuhusu hatari ya kimataifa Control Risks, Bw. Friederike Lyon, amesema kuna uwezekano mdogo kwa Kenya kushuhudia hatari kubwa za kiusalama katika siku za usoni, lakini inatakiwa kuchukua tahadhari na kuimarisha ulinzi ili kuzuia mashambulizi yanayofanywa na kundi la kigaidi la Al-Shabab lenye makao makuu nchini Somalia.

    Bw. Lyon amesema kundi la Al-Shabab litaweza kufanya mashambulizi madogo madogo kwenye sehemu za kaskazini mashariki mwa Kenya katika siku zijazo, kwa hivyo kuna haja ya kuchukua tahadhari ya juu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako