• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yailaani Marekani kwa "ubabe wa kiteknolojia" kwa mpango wa kumkamata ofisa wa fedha wa Huawei

    (GMT+08:00) 2019-01-24 09:09:30

    China imesema mpango wa Marekani kutaka ofisa mkuu wa fedha wa kampuni ya Huawei Bibi Meng Wenzhou kusafirishwa kutoka Canada kwenda Marekani hauendani na sheria za kimataifa na sio halali. Akiongea kwenye mkutano na waandishi wa habari msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bibi Hua Chunying amesema:

    "ombi la Marekani kutaka Bibi Meng asafirishwe kutoka Canada linahusiana na vikwazo vya Marekani dhidi ya Iran. Kampuni ya Huawei imesema mara nyingi kuwa inafuata sheria zote na kanuni za nchi inakofanya kazi. China inapinga Marekani kuchukua hatua za upande mmoja dhidi ya Iran nje ya mpango wa Umoja wa mataifa, kitendo ambacho ni kinyume na sheria za kimataifa na kinapingwa na dunia, ikiwa ni pamoja na washirika wa Marekani. Canada pia inapinga vitendo hivyo."

    Amesema watu wenye welewa na moyo wa kupenda haki kwenye jumuiya ya kimataifa wanatakiwa kupinga vikali kitendo hicho.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako