• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Algeria na Mali zaimarisha ushirikiano wa usalama kwenye mpaka wa pamoja

    (GMT+08:00) 2019-01-24 09:15:41

    Algeria na Mali zimeeeleza dhamira ya kuimarisha ushirikiano wa usalama kwenye mpaka wao, katika kamati ya pamoja ya nne ya usalama iliyozinduliwa nchini Algeria.

    Katibu mkuu wa wizara ya mambo ya ndani ya Algeria Bw Salaheddine Dahmoun akihutubia ufunguzi wa mkutano huo amesema, kiwango cha ushirikiano na mawasiliano kati ya Algeria na Mali kinapaswa kuimarishwa, kwa kuwa mapendekezo yaliyotolewa na mikutano ya awali bado hayajatekelezwa.

    Amesisitiza kuwa Algeria na Mali ziko katika eneo linalotatizwa na vitendo vya ugaidi na uhalifu, hususan usafirishaji wa silaha na dawa za kulevya. Amezihimiza nchi zote mbili kuimarisha ushirikiano, na kupambana na ugaidi, uhalifu, itikadi kali za makundi ya kigaidi, ili kulinda utulivu na usalama kwenye kanda hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako