• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kikosi cha Nigeria chawaangamiza majambazi 58 katika sehemu ya kaskazini ya nchi

    (GMT+08:00) 2019-01-24 09:31:41

    Kikosi cha Nigeria kimewaua majambazi 58 wenye silaha na kuwaokoa mateka 75 katika operesheni zilizofanywa hivi karibuni katika maeneo yenye vurugu ya jimbo la Zamfara, kaskazini mwa nchi hiyo.

    Msemaji wa jeshi hilo Bw. Clement Abiade amesema, kikosi cha operesheni ya Sharan Daji kilifanya mapigano na kundi kubwa la majambazi wenye silaha katika misitu ya Dumburum na Gando jimboni humo.

    Bw. Abiade amesema, kikosi hicho kimewaua majambazi 58 na kumkamta mmoja hai katika mapagano makali yaliyodumu saa kadhaa.

    Pia ameongeza kuwa askari wawili na wanamgambo wawili wameuawa katika mapigano hao, huku askari wengine 8 na wanamgambo 6 wamepata majeruhi ya risasi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako