• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mjasiriamali wa Afrika Kusini aliyetuhumiwa kufadhili ugaidi nchini Msumbiji afariki kifungoni

    (GMT+08:00) 2019-01-24 09:33:28

    Mjasiriamali wa Afrika Kusini Bw. Andrew Hanekom aliyetuhumiwa kufadhili mashambulizi ya kigaidi katika jimbo la Cabo Delgado lililoko kaskazini mwa Msumbiji, amefariki katika hospitali ya kijimbo huko Pemba, mji mkuu wa jimbo hilo.

    Binti wa Bw. Hanekom Bi Amanda Hanekom ametoa taarifa kupitia mtandao wa kijamii ikisema, baba yake amefariki kutokana na chanzo kisichojulikana katika hospitali huko Pemba. Kesi yake itasikilizwa wiki ijayo na angeshinda kesi hiyo, wana ushahidi mwingi wa kuthibitisha yeye hana hatia yoyote.

    Mkewe Bi Francis amefanya kampeni kwa ajili ya kuachiwa kwake tangu akamatwe Agosti iliyopita na amewaambia wanahabari kuwa mumewe hana hatia yoyote lakini imechelewa kuthibitisha hali hiyo, na jambo la pekee linalofuatiliwa naye ni kusafirisha mwili wa mumewe nchini Afrika Kusini.

    Bw. Hanekom mwenye umri wa miaka 62 alimiliki kampuni ya uchukuzi wa baharini huko Cabo Delgado, ambaye alikamatwa baada ya maofisa wa polisi waliofanya doria kujaribu kumlazimisha kuondoka barabarani na kumpiga risasi mkononi na tumboni.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako