• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: CAF yaiondoa klabu ya Ismaily ligi ya mabingwa Afrika

    (GMT+08:00) 2019-01-24 09:42:27

    Shirikisho la soka Afrika (CAF) limeiondoa klabu ya Ismaily ya Misri kushiriki mashindano ya ligi ya mabingwa Afrika, hatua ya makundi.

    CAF imeiandikia klabu hiyo barua kutokana na mashabiki wa Ismailia kufanya vurugu kwa kurusha mawe na chupa za maji wakati wa mechi namba 96 ambapo timu hiyo ilikuatana na klabu Africa ya Tunisia Januari 18 mwaka huu mjini Ismailia Misri.

    Mwamuzi wa mchezo huo alilazimika kumaliza mechi dakika chache kabla ya mechi kuisha kutokana na mashabiki wake kumvamia mwamuzi msaidizi, wachezaji na benchi la ufundi kwa mawe na chupa za maji.

    Kutokana na barua hiyo, sasa kundi C la michuano hiyo linabaki na timu za CS Constantinois inayoongoza kundi hilo ikiwa na pointi 6, Club Africa inashika nafasi ya pili na TP Mazembe inayoshika nafasi ya tatu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako