• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: FIFA yampiga pini maisha Wambura kujihusisha na soka

    (GMT+08:00) 2019-01-24 09:42:55

    Kamati ya nidhamu ya shirikisho la soka duniani (FIFA) limemfungia maisha, Michael Richard Wambura kujihusisha na masuala yote yanayohusiana na mpira wa miguu.

    Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na shirikisho la soka Tanzania (TFF) imesema uamuzi wa kufungiwa kwa Wambura umetolewa januari 22 mwaka huu.

    Kamati ya nidhamu ya FIFA chini ya mwenyekiti wake Anin Yeboah wa Ghana imegongelea nyundo hukumu ya kamati ya rifani ya maadili ya TFF iliyotolewa April 16 mwaka jana. TFF tayari imeshamkabidhi Wambura aliyekuwa makamu wa rais wa shirikisho hilo barua rasmi ya uamuzi wa FIFA.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako