• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Michuano ya SportPesa 2019- Mbao FC yaivua ubingwa Gor Mahia, Wekundu wa Msimbazi na Bandari FC zatinga nusu fainali

    (GMT+08:00) 2019-01-24 09:43:12

    Timu ya Mbao FC ya Tanzania imetinga nusu fainali ya mashindano ya SportPesa baada ya kuwabwaga mabingwa watetezi Gor Mahia ya Kenya kwa jumla ya penalti 4-3 kufuatia kufungana bao 1-1 katika dakika 90 za mchezo. Ikishangiliwa na mashabiki wa Simba na Yanga, Mbao ilionyesha kandanda safi hasa kipindi cha pili.

    Timu nyingine ya Tanzania Simba Sports Club aka Wekundu wa Msimbazi nao wametinga nusu fainali baada ya kuitoa AFC Leopards ya Kenya kwa mabao 2-1.

    Simba sasa itakutana na Bandari FC ya Kenya katika mchezo wa nusu fainali, huku Mbao FC wao watakutana na Kariobangi Sharks ya Kenya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako