• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Spika wa Baraza la Wawakilishi la Marekani amwambia Trump hakuna hotuba ya kitaifa kabla ya kufunguliwa kwa serikali

    (GMT+08:00) 2019-01-24 09:45:20

    Spika wa Baraza la Wawakilishi nchini Marekani Bibi Nancy Pelosi amesema hatamwalika rais Donald Trump kutoa hotuba ya kitaifa kabla ya kufunguliwa kwa idara za serikali, hii ikionyesha kuwa anakataa nia ya rais Trump ya kutoa hotuba Januari, 29. Bibi Pelosi ametoa kauli hiyo baada ya rais Trump kusema kwenye barua yake kuwa anatarajia kutoa hotuba Bungeni katika Baraza la Wawakilishi Januari, 29. Ni siku ya 33 baada ya kufungwa kwa baadhi ya idara za serikali ya Marekani, kitu ambacho kimezushwa na mzozo kati ya vyama juu ya madai ya rais Trump ya pesa za kujenga ukuta wa mpakani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako