• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kuwa soko kubwa la manunuzi duniani kwa mwaka huu

    (GMT+08:00) 2019-01-24 19:15:30

    Kampuni ya utafiti ya eMarketer imetoa ripoti ikisema, China inaweza kuipita Marekani na kuwa soko kubwa zaidi la manunuzi duniani kwa mwaka huu.

    Ripoti hiyo imekadiria kuwa mauzo ya rejareja nchini China yatakua kwa asilimia 7.5 na kufikia dola za kimarekani trilioni 5.636 kwa mwaka huu, huku mauzo hayo kwa Marekani yakikua kwa asilimia 3.3 na kufikia dola trilioni 5.529.

    Ripoti hiyo imeeleza sababu ya ukuaji huo kuwa ni kuongezeka kwa kipato cha raia na kushamiri kwa biashara kupitia mtandao wa internet, ambayo ni kichocheo kikubwa cha uchumi wa China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako