• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kigali kuwa mwenyeji wa mkutano wa biashara Afrika

  (GMT+08:00) 2019-01-24 20:01:38

  Viongozi wa biashara zaidi ya 1500 kutoka kote barani Afrika wanatarajiwa kukongamana jijini Kigali mwezi Machi kujadiliana kuhusu ushirikiano wa kiuchumi wa Afrika.

  Mkutano huo uliopewa jina "Mkutano wa Mkurugenzi Mtendaji 2019",katika makala yake ya 7 huwaleta pamoja viongozi wa biashara kujadili masuala mbalimbali ya uchumi.

  Kulingana na taarifa,mkutano wa mwaka huu utafanyika tarehe 25 na 26 Machi.

  Washiriki ni pamoja na waamuzi kutoka sekta ya baishara,fedha na siasa,kutoka nchi zaidi ya 70 kujadili ushirikiano wa kikanda pamoja na masuala mengine ya kukuza biashara Afrika.

  Ajenda kuu katika mkutano huo itakuwa ni utekelezwaji wa eneo la biashara huru barani Afrika (CFTA) ,kichocheo kikuu cha ukuaji wa sekta binafsi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako