• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania kupata ongezeko la asilimia 50 la watalii kutoka China 2019

    (GMT+08:00) 2019-01-24 20:06:35

    Kutokana na jitihada zilizofanywa na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) idadi ya watalii kutoka China nchini Tanzania inatarajiwa kuongezeka kwa asilimia 50 katika mwaka huu wa 2019.

    Bodi ya TTB ilifanya juhudi kubwa katika kuvitangaza vivutio vya utalii pamoja na Shirika la ndege la ATCL baada ya watendaji wa Bodi hiyo kuzuru China mwezi Novemba mwaka jana.

    Aidha wakati huo bodi ya TTB iliingia makubaliano na kusaini mkataba na kampuni ya China ya Touchroad International Holdings Group ambayo iliahidi kupeleka watalii 10,000 Tanzania.

    Mkurugenzi wa TTB,Devotha Mdachi alisema makubaliano hayo yanalenga kuisaidia Tanzania kutangaza vivutio vyake vya utalii China ili kupata wageni wengi kutoka nchi hiyo.

    Takwimu za Wizara ya Utalii Tanzania zinaonyesha kuwa nchi hiyo hupata wastani wa watalii 20,000 kila mwaka kutoka China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako