• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • RwandAir kununua ndege mpya

  (GMT+08:00) 2019-01-24 20:07:29

  Shirika la ndege la Rwanda,RwandAir linapanga kuongeza idadi ya ndege ili kuhudumia njia nyingine katika ukanda wa Afrika na njia nyingine duaniani ikiwa ni pamoja na New York na China.

  Mkurugenzi Mtendaji wa RwandAir,Yvonne Manzi Makolo, amesema kuwa wako katika mchakato wa kununua ndege nyengine zaidi ili kusaidia katika mkakati wa upanuzi wa shirika hilo.

  RwandAir tayari inaendesha ndege 12 ambapo mbili ni za aina ya Airbus A330s, sita ni Boeing 737NGs, mbili ni Bombardier CRJs, na mbili Q400s.

  Idadi hii ya ndege huenda ikaongezeka hivi karibuni iwapo mipango ya shirika hilo ya kununua ndege nyengine itafanikiwa.

  Hii inatarajiwa kuliweka shirika hilo katika nafasi nzuri ya mipango yake ya upanuzi katika sekta iliyo na ushindani mkubwa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako