• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kushikilia kuhimiza kufungua mlango kwa pande zote na kuhimiza ushirikiano wa kimataifa wa "Ukanda Mmoja na Njia Moja"

    (GMT+08:00) 2019-01-24 20:50:15

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bibi Hua Chunying leo hapa Beijing amesema, China siku zote inaunga mkono, kulinda na kutekeleza utaratibu wa pande nyingi, na itashikilia kufungua mlango kwa pande zote, kuhimiza ushirikiano wa kimataifa wa "Ukanda Mmoja na Njia Moja", na kujenga uchumi wa dunia wa wazi na wa kiwango cha juu zaidi.

    Habari zinasema, mkurugenzi mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa mjini Geneva Bw. Michael Møller amesema, China ni muhimu katika kulinda utaratibu wa pande nyingi. Amekumbushia hotuba iliyotolewa mwanzoni mwa mwaka 2017 na rais Xi Jinping wa China, ambapo alisisitiza kuunga mkono utaratibu wa pande nyingi. Amesema Katika miaka miwili iliyopita, China imetumia vitendo halisi kuonyesha uungaji mkono kwa utaratibu huo.

    Bibi Hua Chunying amesema, China inashikilia kujenga uchumi wa dunia wa wazi na wa kiwango cha juu zaidi, kutumia wazo la kujadiliana na kunufaishana, na kujenga uhusiano wa kimataifa wa aina mpya wa kuheshimiana, haki na usawa, na kunufaishana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako