• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Huawei yakiidhinisha chuo Kikuu cha CUEA cha Kenya kuwa kituo cha kitaaluma

    (GMT+08:00) 2019-01-25 09:07:49

    Kampuni ya mawasiliano ya simu ya China Huawei jana imekiidhinisha chuo kikuu cha CUEA cha Kenya kuwa kituo cha kitaaluma kitakachotoa mafunzo ya Tehama.

    Akiongea kwenye sherehe Makamu Mkuu wa Chuo cha CUEA Stephen Mbugua, amepongeza ushirikiano na kueleza matumaini yake kwamba kitasaidia kuimarisha mafunzo ya wanafunzi wa sayansi ya compyuta. Kutokana na mkataba wa makubaliano, chuo hicho sasa kimeidhinishwa na Huawei kutoa mafunzo rasmi ya kiufundi na kutoa vyeti kwa wanafunzi wake wakitumia mtaala na vifaa vya mafunzo vilivyoidhinishwa na Huawei. Mbugua amesema ushirikiano na kampuni hiyo ya China utafika mbali katika kujenga watu wenye ujuzi wa Tehama katika Afrika.

    Naye meneja mafunzo na vyeti wa Huawei Su Shuqi, amesema mafunzo hayo yatasaidia sana kupunguza mwanya kati ya taaluma na viwanda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako