• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudan Kusini yasema inashirikiana na EAC kurahisisha usafiri, na biashara

    (GMT+08:00) 2019-01-25 09:08:08

    Sudan Kusini imesema inashughulikia pendekezo la baraza la biashara la Afrika Mashariki ili kurahisisha usafiri na gharama wanapofanya biashara ndani ya kanda hiyo.

    Akiongea na wanahabari mjini Juba waziri wa biashara na mambo ya Afrika Mashariki Paul Mayom Akech, amesema nchi tano wanachama zikiwemo Uganda, Kenya, Tanzania, Rwanda na Burundi zimekubali kutoa viza bure ili kurahisisha usafiri kwa Wasudan Kusini ndani ya kanda hiyo, na kwamba hivi sasa wanashughulikia viza. Amesema wamejadiliana na wizara ya mambo ya nje pamoja na ya ndani na kwamba nyaraka husika zinafanyiwa utaratibu.

    Kwa upande wake Katibu mkuu msaidizi wa wizara ya biashara na mambo ya Afrika Mashariki, Mou Mou Athian Kuol, amesema wamedhamiria kufikia masharti ya uanachama wa jumuiya hiyo kutokana na ugumu wa uchumi uliosababishwa na mgogoro uliodumu kwa miaka mitano.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako