• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania imewatia mbaroni wageni 198 katika msako dhidi ya uvuvi haramu

    (GMT+08:00) 2019-01-25 09:08:28

    Takriban wageni 198 wametiwa mbaroni wakihusishwa na uvuvi haramu katika Ziwa Tanganyika tangu mamlaka za Tanzania zianzishe msako mkubwa dhidi ya uvuvi haramu kwenye ziwa hilo.

    Akihojiwa na shirika la habari la China Xinhua, Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Emmanuel Maganga, amesema Watanzania 284 pia wametiwa mbaroni na nyavu 11,529 za uvuvi haramu zimekamatwa katika kampeni hiyo iliyoanzia mwezi Novemba mwaka jana. Amefafanua kuwa mamlaka zinafanya mpango wa kuwashtaki watuhumiwa mahakamani, na kuongeza kuwa mbali na uvuvi haramu, watuhumiwa hao pia watashtakiwa kwa kuvua samaki wachanga.

    Akizindua msako huo Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina, amesema msako huo pia utalenga kuwakamata maofisa wa serikali na maofisa wa uvuvi wanaowalinda watu wanaohusika na uvuvi haramu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako