• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Idadi ya vifo kwenye maandamano Sudan yafikia 29

    (GMT+08:00) 2019-01-25 09:17:57

    Idadi ya vifo vinavyotokana na maandamano makubwa nchini Sudan imeongezeka hadi kufikia 29.

    Mkuu wa Kamati Kuu ya Sudan inayoshughulikia uchunguzi wa maandamano yaliyotokea hivi karibuni nchini Sudan Bw. Amer Mohamed Ibrahim amesema, mpaka sasa idadi ya vifo imefikia 29 tangu maandamano hayo yaanze Desemba 19 mwaka jana.

    Ameeleza kuwa vifo vya watu tisa viliripotiwa katika jimbo la Gadarif, sita katika jimbo la Nahral-Neel, na vitatu katika jimbo la White Nile, pia katika jimbo la Kaskazini vimeripotiwa vifo vitatu, vinne katika Omdurman na vingine vinne huko Khartoum.

    Bw. Ibrahim pia ametangaza kuwa mwandamanaji mmoja mwenye umri wa miaka 24 ameuawa katika maandamano ya Alhamisi huko Khartoum.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako