• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • MBIO ZA MAGARI: KBC yatoa udhamini wa shilingi milioni 75

    (GMT+08:00) 2019-01-25 09:20:31

    Benki ya KCB ya Kenya imerejea katika mashindano ya mbio za magari kwa kishindo baada ya kutangaza itakuwa mdhamini mkuu wa mashindano ya mwaka huu, mwaka 2020 na 2021 na kumwaga shilingi milioni 75 katika makala hayo matatu.

    Kila mwaka, benki hiyo imesema itatumia shilingi milioni 20 kuandaa duru za mbio za kitaifa za magari (KNRC) na shilingi milioni 5 kwa mashindano ya vigari vya Autocross. Mashindano haya mawili sasa yatatumia majina KCB Bank Rally na KCB Bank Autocross.

    Ikitangaza udhamini kwa Shirikisho la mashindano ya mbio za magari la Kenya (KMSF), KCB imesema kutakuweko na duru saba za mbio za magari na duru 10 za Autocross mwaka huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako