• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Katibu mkuu wa UM afuatilia vurugu nchini Venezuela

    (GMT+08:00) 2019-01-25 09:27:36

    Msemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Stephane Dujarric, ametoa taarifa akisema katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres anafuatilia vurugu nchini Venezuela na kutoa wito wa kupunguza hali ya wasiwasi.

    Bw. Guterres pia ametaka kufanyika kwa uchunguzi wa wazi na huru kuhusu matukio yaliyotokea nchini humo, na pia amesisitiza kuwa wahusika wote wa matukio hayo wanahitaji kufanya mazungumzo shirikishi na ya kuaminika ya kisiasa ili kushughulikia mgogoro wa muda mrefu nchini humo, na kuheshimu vya kutosha kanuni za sheria na haki za binadamu.

    Habari nyingine zinasema, baada ya nchi nyingine kumtambua spika wa bunge la Venezuela Bw. Juan Guaido, ambaye amejitangaza kama rais wa mpito wa nchi hiyo Jumatano wiki hii, rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki ameeleza kumuunga mkono Bw. Nicolas Maduro wa Venezuela.

    Naye Rais Vladimir Putin wa Russia ametangaza kuiunga mkono serikali halali kwenye mazungumzo ya simu kati yake na kiongozi wa Venezuela Bw. Nicolas Maduro.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako