• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Namibia kuwa mwenyeji wa mkutano wa kimataifa kuhusu uhaba wa maji na umeme wa maji barani Afrika

    (GMT+08:00) 2019-01-25 09:45:26

    Wataalamu wa nishati wa kimataifa watakutana kwenye mkutano utakaofanyika huko Windhoek, mji mkuu wa Namibia, kujadili upungufu wa maji na maendeleo ya umeme wa maji barani Afrika.

    Mkutano huo unaandaliwa na Shirika la Aqua Media International, ambalo ni mchapishaji wa jarida la kimataifa kuhusu umeme wa maji na mabwawa ya maji, lenye wasomaji katika nchi 180 kote duniani.

    Wizara za kilimo, madini na nishati, pamoja na mamlaka za maji na nishati nchini Namibia zinatarajiwa kushiriki kwenye mkutano huo, pamoja na wajumbe waandamizi kutoka sehemu mbalimbali duniani.

    Kwa mujibu wa waandaaji wa mkutano huo, wajumbe 650 kutoka nchi 50 watafuatilia masuala ya maji na umeme wa maji barani Afrika, yakiwemo ya kiufundi, kifedha, kimazingira na kijamii.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako