• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • WFP yapokea mchango wa dola milioni 4.5 wa kutoa msaada wa kibinadamu Sudan Kusini

    (GMT+08:00) 2019-01-25 09:45:45

    Shirika la mpango wa chakula duniani WFP limesema kuwa limepokea mchango wa ziada wa dola milioni 4.5 za kimarekani kwa ajili ya kutoa msaada wa kibinadamu kwa watu zaidi ya milioni 7 wanaokabiliwa na uhaba wa chakula nchini Sudan kusini.

    Kaimu mkurugenzi wa WFP nchini Sudan kusini Bw. Simon Cammelbeeck amesema fedha hizo kutoka Ujerumani pia zitaziwezesha ndege za Umoja wa mataifa kuendelea kutoa huduma za usafiri kwenye maeneo yenye mahitaji ya kibinadamu.

    Amesema fedha hizo zitatumika kutoa msaada wa chakula na lishe kwa watu wenye mahitaji, wakiwemo wakimbizi na watoto chini ya miaka miwili kote nchini humo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako