• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • DRC yashuhudia ongezeko kubwa la maambukizi ya Ebola kwa siku

    (GMT+08:00) 2019-01-25 09:46:04

    Matukio 14 ya maambukizi mapya ya homa ya Ebola yameripotiwa kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo DRC Jumatano, idadi ambayo ni ongezeko kubwa zaidi kwa siku tangu homa hiyo ilipuke mwezi Agosti mwaka jana.

    Naibu msemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Bw. Farhan Haq amesema Tisa kati ya matukio hayo mapya yamegunduliwa karibu na Butembo, mji wenye watu milioni moja, na mpaka sasa idadi ya maambukizi yaliyothibitishwa na matukio yanayoshukiwa kuwa ni maambukizi imefikia 699, wakiwemo wahanga 433 waliofariki dunia.

    Bw. Haq amesema wizara ya afya ya DRC, Shirika la afya duniani WHO na wadau wa kibinadamu wameimarisha hatua za kukabiliana na homa hiyo, na kupungua kwa matukio ya Ebola kumeripotiwa Beni, mji ambao ulikuwa ni chimbuko la mlipuko wa homa hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako