• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • AMISOM yataka kuvipanga upya vikosi vyake kabla ya kuondolewa kwa wanajeshi wa Burundi

    (GMT+08:00) 2019-01-25 09:55:58

    Tume ya Umoja wa Afrika nchini Somalia AMISOM imesema inataka kuvipanga upya vikosi vyake na jeshi la Somalia SNA kabla ya kuondolewa kwa wanajeshi 1,000 kutoka kikosi cha Burundi mwezi ujao.

    Akihutubia mkutano wa usalama mjini Mogadishu, Mjumbe maalumu wa mwenyekiti wa Kamati ya Umoja wa Afrika nchini Somalia Bw Francisco Madeira amesisitiza kuwa ni muhimu kwa jeshi la umoja huo kufanya operesheni ya kijeshi ya pamoja, ili kuwaangamiza waasi wa Kundi la al-Shabab nchini Somalia.

    Madeira amesema, kipindi cha mpito ni njia yenye ufanisi katika utaratibu wa usimamizi wa mamlaka za serikali, ili kuhakikisha amani na usalama nchini Somalia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako