• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nia ya kisiasa ya kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa ni dhaifu

    (GMT+08:00) 2019-01-25 19:21:17

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres amesema, mabadiliko ya hali ya hewa ni tishio dhahiri kwa dunia, lakini nia ya kisiasa ya kukabiliana na tishio hilo ni dhaifu.

    Akizungumza kwenye mkutano wa mwaka 2019 wa Baraza la Uchumi la Dunia hapo jana, Bw. Guterres amesema, dunia inakabiliwa na matishio mengi ikiwemo mgogoro wa biashara, suala la madeni na kutokuwa na utulivu kwa soko la fedha, lakini mabadiliko ya hali ya hewa ni tishio kubwa kuliko inavyodhaniwa na wanasayansi.

    Amesema ili kupata uungaji mkono wa watu kwa utaratibu wa pande mbalimbali na Umoja wa Mataifa, umoja huo unapaswa kutilia maanani watu wanaopinga utaratibu huo na kuona wametupwa, kuwasaidia kutatua matatizo na pia kuwaelewesha kuwa Umoja wa Mataifa unafanya mageuzi halisi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako