• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yapinga kitendo cha kuingilia kati mambo ya ndani ya Venezuela

    (GMT+08:00) 2019-01-25 19:36:30

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bibi Hua Chunying amesema, , China inapinga nchi nyingine kuingilia kati mambo ya ndani ya Venezuela, hasa kutishia kuingilia kwa nguvu ya kijeshi, na kwamba mambo ya Venezuela ni lazima kuchaguliwa na kuamuliwa na watu wa nchi hiyo.

    Bibi Hua Chunying amesema, China inatetea nchi zote kufuata lengo na kanuni ya katiba ya Umoja wa Mataifa, hasa kutoingiliana mambo ya ndani, kuheshimu mamlaka na ukamilifu wa ardhi, kutotishia kwa nguvu ya kijeshi, na kanuni nyingine za uhusiano wa kimataifa na sheria za kimataifa. Amesisitiza kuwa, China inazitaka pande mbalimbali kuheshimu matakwa ya watu wa Venezuela, kuunga mkono pande mbalimbali za nchi hiyo kutafuta utatuzi wa kisiasa kwa njia ya mazungumzo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako