• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sakata la trilioni 1.5 laanza kufanyiwa kazi Tanzania

    (GMT+08:00) 2019-01-25 20:18:53

    Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali nchini Tanzania (PAC) imeanza kulifanyia kazi sakata la Sh1.5 trilioni.

    Hatua hiyo imekuja baada ya kamati hiyo kukutana na ofisi ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) mjini Dodoma huku Spika wa Bunge la Tanzania Job Ndugai akisema kuwa mwenyekiti wa kamati hiyo atatoa taarifa ya mwaka ya kamati yake katika mkutano wa Bunge unaotarajiwa kuanza wiki ijayo.

    Sakata la fedha hizo liliibuliwa na mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe alipokuwa akichambua ripoti ya CAG ya 2016/17.

    Sakata hilo ambalo tangu lilipoibuliwa Serikali imeendelea kusema italitolea ufafanuzi katika kamati ya PAC.

    Suala la fedha hizo ambazo Zitto alidai hazionekani jinsi zilivyotumika katika ripoti ya CAG, lilipata ufafanuzi Aprili 20, mwaka jana wakati Rais John Magufuli akiwaapisha majaji wapya Ikulu jijini Dodoma.

    Rais Magufuli alisema hakuna fedha iliyoliwa na kama ingekuwa hivyo, basi watendaji waliohusika angewachukuliwa hatua.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako