• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UM kuwekeza kwenye sekta ya nyumba Kenya

    (GMT+08:00) 2019-01-25 20:20:18

    Umoja wa mataifa umesema utakusanya jumla ya shilingi bilioni 64.7 kwa ajili ya kujenga nyumba laki moja nchini Kenya kupiga jeki mpango wa serikali wa kujenga nyumba za gharama ya chini. UM umesema utawekeza shilingi bilioni 1 kuanza mradi huo na utahimiza mashirika mengine kuchangia katika uwekezaji huo.

    Tangazo hilo linafuatia makubaliano yaliyosainiwa katika kikao cha 73 za UM mjini New York Marekani Septemba mwaka jana pamoja na serikali ya kujenga nyumba laki moja za gharama nafuu. Ofisi ya UM ya kushughulikia miradi UNOPS imesema nyumba hizo zitatumiwa malighafi ambayo yatachangia juhudi za kulinda mazingira. Nyumba hizo pia zitatumia malighafi ya Kenya jambo ambalo litatoa ajira kwa wenyeji na kuchangia ukuaji wa uchumi wa nchi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako