• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Maduro asema Venezuela itadumisha uhusiano wa kiuchumi na kibiashara na Marekani

    (GMT+08:00) 2019-01-26 16:19:56

    Rais Nicolás Maduro wa Venezuela amesema, licha ya kukatisha uhusiano wa kibalozi na Marekani, Venezuela itadumisha uhusiano wa kiuchumi na kibiashara na Marekani, vilevile amekitaka chama cha upinzani kifanye mazungumzo na serikali ili kutatua mgongano.

    Rais Maduro ameilaani Marekani kufanya mapinduzi ya kisiasa nchini Venezuela, amesisitiza kuwa wafanyakazi wote wa ubalozi wa Marekani nchini Venezuela lazima waondoke ndani saa 72. Amesema ingawa serikali ya Venezuela imesitisha uhusiano wa kisiasa na kibalozi na Marekani, lakini bado itadumisha uhusiano wa kiuchumi na kibiashara na Marekani. Vilevile amesema, njia ya mazungumzo kati ya serikali na chama cha upinzani ni ya wazi, anapenda kufanya mazungumzo na kiongozi wa wapinzani Bw. Juan Guaido.

     

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako