• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa mataifa wajadili madhara ya mabadiliko ya hali ya hewa na kutaka hatua zichukuliwe

    (GMT+08:00) 2019-01-26 16:22:39

    Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limefanya mjadala wa wazi kuhusu madhara ya mabadiliko ya hali ya hewa kwa amani na usalama, na kutoa mwito wa kupunguza madhara ya mabadiliko ya hali ya hewa. Ofisa wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia mambo ya kisiasa Bibi Rosemary DiCarlo, amesema hatari zinazotokana na majanga yanayohusiana na mabadiliko ya hali ya hewa, tayari ni hali halisi kwa dunia ya sasa, na hatari hizo zinawakumba mamilioni ya watu duniani.

    Bibi DiCarlo amesema kwa sasa jambo la muhimu zaidi ni kuhakikisha kuwa ahadi zinafuata vitendo. Tayari majeshi makubwa na biashara kubwa zimetambua haja ya kujiandaa kukabiliana na hatari zinazotokana na mabadiliko ya hali ya hewa.

    Ofisa wa Shirika la mipango ya maendeleo la Umoja wa mataifa Bw Achim Steiner, amesema mabadiliko ya hali ya hewa hayaleti madhara kwa hewa peke yake, bali pia yanaleta madhara kwa viumbe, na kusema dunia bado haijapambana vya kutosha na mabadiliko hayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako