• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Donald Trump asaini amri ya kusitisha kwa muda kufungwa kwa baadhi ya idara za serikali

    (GMT+08:00) 2019-01-26 16:23:53

    Serikali ya Marekani imefunguliwa jana baada ya Rais Donald Trump kusaini muswada wa kuipatia serikali fedha kwa muda wa wiki tatu. Taarifa iliyotolewa na ikulu ya Marekani inasema muswada huo utaipatia fedha serikali hadi tarehe 15 ya mwezi huu.

    Kwenye muswada huo hakuna pesa ambazo Rais Trump alizitaka kwa ajili ya ujenzi wa ukuta kwenye mpaka na Mexico, na kusema chama cha Democrats na Republican wataendelea na majadiliano kuhusu usalama mpakani kwa muda wa wiki tatu.

    Muswada huo umekuja baada ya miswada miwili iliyokubaliwa na Ikulu ya Marekani na chama cha Democrat, kukataliwa na baraza la Seneti.

    Mgawanyo mkubwa ndani ya chama cha Republican, na kuahirishwa kwa ndege nyingi mjini New York kutokana na kutokuwepo kwa wafanyakazi wa usimamizi wa usalama wa ndege, kumemfanya Rais Trump alegeze msimamo wake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako