• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baraza la usalama lafanya mkutano wa dharura kuhusu hali ya Venezuela

    (GMT+08:00) 2019-01-27 16:23:56

    Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa jana lilifanya mkutano wa dharura kuhusu hali ya Venezuela. Naibu katibu mkuu wa umoja huo anayeshughulikia mambo ya siasa na ulinzi wa amani Bi. Rosemary DiCarlo na balozi wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Bw. Ma Zhaoxu wameitaka jumuiya ya kimataifa itafute mpango wa utatuzi wa kisiasa kwa hali ya sasa ya Venezuela.

    Bi. DiCarlo ameitaka jumuiya ya kimataifa ifanye juhudi ili kuzuia hali ya Venezuela isizidi kuwa mbaya, na kuhakikisha wavenezuela wana haki zote za binadamu.

    Balozi Ma Zhaoxu amesema China inaiunga mkono serikali ya Venezuela kwa juhudi zake za kulinda mamlaka, uhuru na utulivu wa taifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako