• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • RIADHA: Ethiopia haikamatiki katika riadha wanaume, Chepng'etich wa Kenya ashinda kwa wanawake.

    (GMT+08:00) 2019-01-28 08:26:20
    Ruth Chepng'etich amepeperusha vyema bendera ya Kenya baada ya kunyakua taji lake la kwanza la Dubai Marathon baada ya ukame wa miaka 12 kwa kutimua mbio kwa saa 2:17:07 mashindano yaliyofanyika Dubai.

    wanariadha wawili wa Ethiopia Worknesh Degefa na Worknesh Edesa wamekamata nafasi ya pili na tatu kwenye mashindao hayo upande wa wanawake.

    upande wa wanaume, Getaneh Molla wa Ethiopia amechukua taji baada ya kutumia masaa 2:03:34 ambayo ni kasi ya juu zaidi ya mkimbiaji anayeshiriki marathoni kwa mara yake ya kwanza. nafasi ya pili na ya tatu imekwenda kwa Waethiopia wengine Hepassa Negasa na Afesa Mengstu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako