• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping wa China akutana na ofisa mwanadamizi wa Korea Kaskazini

    (GMT+08:00) 2019-01-28 08:42:41

    Rais Xi Jinping wa China na mke wake Bibi Peng Liyuan jana hapa Beijing walikutana na ofisa mwandamizi kutoka Korea Kaskazini Bw. Ri Su Yong, na pia walitazama kwa pamoja maonesho yaliyofanywa wasanii wa Korea Kaskazini.

    Bw. Ri ambaye ni mjumbe wa ofisi ya kisiasa ya Kamati kuu ya chama cha wafanyakazi cha Korea Kaskazini, naibu mwenyekiti wa kamati kuu ya chama na mkurugenzi wa idara ya mahusiano ya kimataifa ya Chama, anaongoza ujumbe wa wasanii kwenye ziara nchini China, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya sherehe za miaka 70 ya uhusiano wa kibalozi kati ya China na Korea Kaskazini.

    Kwenye mazungumzo yao rais Xi Jinping amesema yeye na mwenzake wa Korea Kaskazini Kim Jong Un wamefikia makubaliano muhimu kuhusu maendeleo ya uhusiano kati ya pande hizo mbili kwenye zama mpya katika mikutano yao minne ya mwaka jana. Amesisitiza kuwa China iko tayari kushirikiana na Korea Kaskazini kutekeleza makubaliano yaliyofikiwa na pande mbili, ili kuwanufaisha zaidi watu wa nchi hizo mbili, na kutoa mchango kwa amani, utulivu, maendeleo na ustawi wa dunia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako