• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Sudan arudi Khartoum baada ya kutembelea Misri

    (GMT+08:00) 2019-01-28 09:02:53

    Rais Omar al-Bashir wa Sudan jana aliwasili mjini Khartoum baada ya kumaliza ziara yake ya siku moja nchini Misri.

    Waziri wa mambo ya nje wa Sudan BwAl-Dirdiri Ahmed amesema ziara ya rais al-Bashiri nchini Misri ni fursa nzuri ya kufuatilia utekelezaji wa miradi mbalimbali iliyofikiwa makubaliano, na kuwa majadiliano kati ya pande mbili yalilenga mambo yanayofuatiliwa kwa pamoja na pande mbili, na maendeleo katika nchi za kiarabu na nchi za Afrika.

    Viongozi hao pia wamejadili ushirikiano wa nchi tatu kati ya Misri, Ethiopia na Sudan kuhusu miradi ya bonde la Nile na bwawa la GERD.

    Akiongea kwenye mkutano wa pamoja na wanahabari na mwenyeji wake kabla ya kuondoka Misri, Rais al-Bashir amesema kuna mashirika hasi yanayofanya kazi ya kuvuruga amani na kuiyumbisha Sudan. Na kusema Sudan inafahamu kuhusu majaribio hayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako