• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya Tanzania yasimamisha kutoa leseni mpya za uwindaji kwa makampuni yaliyopoteza sifa

    (GMT+08:00) 2019-01-28 09:03:13

    Serikali ya Tanzania imetangaza kuwa haitatoa tena vibali vya uwindaji kwa makampuni ya uwindaji kwa watalii, ambayo yameshindwa kuwalipa wanavijiji kwenye maeneo yanakofanya shughuli zao.

    Naibu waziri wa maliasili na utalii wa Tanzania Bw. Constantine Kanyasu amesema mjini Arusha kuwa hakuna leseni za uwindaji zitakazotolewa kwa makampuni ambayo hayajawalipa wanakijiji.

    Kauli ya naibu waziri imekuja baada ya wakazi wa vijiji 23 katika wilaya ya Longido kulalamika kuwa baadhi ya mashirika ya uwindaji yamekiuka mikataba kwa kutozilipa serikali za mitaa. Wawakilishi wa vijiji 23 wamelalamika kuwa wanadai jumla ya dola laki moja na elfu 43 lakini hawajalipwa kama inavyoelezwa kwenye makubaliano.

    Jumla ya makampuni 47 yalipewa leseni za uwindaji, na yanatakiwa kulipa asilimia 25 ya mapato yao kwa vijiji vya maeneo yanakopeleka watalii kuwinda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako