• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wahamiaji 52 haramu wa Afrika waokolewa kwenye pwani ya Algeria

    (GMT+08:00) 2019-01-28 09:20:52

    Habari kutoka vyombo vya habari vya Algeria zinasema jeshi la majini la Algeria limewaokoa wahamiaji 52 haramu wa Afrika kwenye pwani ya magharibi ya Ghazaouet, mkoani Tlemcen.

    Kituo cha televisheni cha ENTV kimesema wahamiaji hao 52 wanatoka nchi tofauti za Afrika, boti yao iliyotengenezwa kwa mikono iliharibika kutokana na dhoruba baharini kwenye sehemu ya kaskazini mwa Algeria, lakini iliokolewa na jeshi la majini la Algeria kwa wakati, lilipokuwa kwenye doria katika sehemu hiyo.

    Huenda Wahamiaji hao walikuwa wanajaribu kwenda Hispania, kwa kuwa pwani ya magharibi ya Algeria ni karibu na peninsula ya Iberia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako