• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Iran yahimiza Umoja wa Ulaya kutimiza ahadi za nyuklia

    (GMT+08:00) 2019-01-28 14:21:34

    Shirika la habari la Iran, IRNA limeripoti kuwa mkurugenzi wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran Bw. Ali Akbar Salehi amehimiza Umoja wa Ulaya (EU) kutekeleza majukumu yake kuhusu makubaliano ya kimataifa ya nyuklia kuhusu Iran.

    Bw. Salehi amezungumzia njia maalum (SPV) ambayo nchi za Ulaya inafikiria kuitumia kufanya biashara na Iran, licha ya vitisho vya Marekani dhidi ya Iran. Amesema kama nchi za Ulaya hazitatekeleza ahadi zao, hatua zinazofuata hazitakuwa nzuri kwa Iran, nchi za Ulaya na hata nchi zilizosaini makubaliano.

    Gazeti la Tehran Times limeripoti kuwa katika mkutano uliofanyika huko Tehran, mkurugenzi wa Chama cha biashara, viwanda, madini na Kilimo (ICCIMA) Bw. Gholam-Hossein Shafeie, na mkuu shirika la Bidhaa za Uturuki (TOBB) Bw. Rifat Hisarciklioglu pia wamejadili njia ya kupanua biashara kati ya pande mbili licha ya vikwazo vya Marekani dhidi ya Iran.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako