• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yasema tuhuma za uongo dhidi ya kampuni ya Huawei ni hatari kwa ushindani huru na wa usawa

    (GMT+08:00) 2019-01-28 19:19:49

    Balozi wa China nchini Uingereza Liu Xiaoming amelaani vikali tuhuma zisizo na msingi dhidi ya kampuni ya mawasiliano ya Huawei ya China, akisisitiza kuwa kampuni hiyo haina tishio lolote kwa nchi yoyote.

    Waraka ulioandikwa na Balozi huyo na kuchapishwa kwenye gazeti la The Telegraph la Uingereza umeeleza kuwa kama tuhuma hizo zisiposhughulikiwa, zinaweza kuvuruga kanuni za soko, kupunguza uaminifu kwa kampuni hiyo, kuharibu ushirikiano wa kibiashara, na kusababisha wasiwasi na kuyumba kwa uchumi wa dunia.

    Balozi huyo amesema, kampuni ya Huawei tawi la Uingereza imetoa mchango muhimu katika maendeleo ya uchumi na jamii ya nchi hiyo katika miaka mitano iliyopita kwa kuingiza paundi bilioni 2 kwa Uingereza kupitia uwekezaji na uwakala, na kutoa nafasi zaidi ya elfu 7 za ajira.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako