• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Venezuela yalaani vikali Umoja wa Ulaya kuitaka kufanya tena uchaguzi wa urais

    (GMT+08:00) 2019-01-28 19:23:08

    Wizara ya mambo ya nje ya Venezuela imetoa taarifa ikilaani vikali Umoja wa Ulaya kuitaka nchi hiyo kufanya tena uchaguzi wa urais.

    Mjumbe wa ngazi ya juu wa sera ya diplomasia na usalama wa Umoja wa Ulaya Bi. Federica Mogherini ameitaka Venezuela kutangaza kufanya tena uchaguzi wa urais, ama sivyo Umoja huo utatambua uhalali wa rais wa muda na mwenyekiti wa bunge la nchi hiyo Bw. Juan Guaido. Ufaransa, Uingereza, Ujerumani, Uhispania, Ureno na Uholanzi pia zimeishinikiza serikali ya nchi hiyo na kuitaka kufanya uchaguzi wa urais ndani ya siku 8.

    Taarifa hiyo imedai kuwa Umoja wa Ulaya umejiunga na mpango wa kupindua serikali ya Venezuela unaopangwa na serikali ya Marekani, hata kutoa kauli ya mwisho kwa nchi hiyo, na kusisitza kuwa uhalali wa serikali ya nchi hiyo hautaathiriwa na nchi za nje.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako