• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yajibu Kauli ya waziri wa mambo ya nje wa Marekani kuhusu hali ya Venezuela

    (GMT+08:00) 2019-01-28 20:52:19

    Msemaji wa Wizara ya Mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang amesema, mambo ya Venezuela ni lazima yapatiwe ufumbuzi na watu wake wenyewe, na kuzitaka pande zote husika zifanye mambo yanayosaidia utulivu na maendeleo ya nchi hiyo.

    Bw. Geng Shuang amesema hayo wakati alipozungumzia kauli za waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo kuhusu hali ya Venezuela aliyoitoa kwenye mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya Venezuela uliofanyika jumamosi iliyopia. Bw. Pompeo amezilaumu China na Russia kwa kulizuia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kupitisha taarifa ya mwenyekiti, akisema nchi hizo mbili zinajaribu kuunga mkono mamlaka ya Maduro "ambayo ni ya kushindwa".

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako