• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • RIADHA: Sumgong aongezewa adhabu hadi 2025 kwa kutoa ushahidi wa uongo wa kutumia Pufa

    (GMT+08:00) 2019-01-29 07:50:49
    Mwanariadha wa Kenya Jemimah Sumgong ameongezwa adhabu ya kufungiwa kujishughulisha na michezo kwa muda wa miaka nane kwa kosa la kutumia dawa za kusisimua misuli (Pufa).

    jopo huru la nidhamu katika shirikisho la riadha duniani (IAAF) limetupilia mbali madai ya mwanariadha huyo kwamba dawa hizo alitumia baada ya daktari feki kumchoma sindano katika hospitali moja wakati madaktari wakiwa kwenye mgomo.

    Hukumu hiyo inamaanisha kwamba Sumgong, mkenya wa kwanza kabisa mwanamke kushinda marathon katika michezo ya Olimpiki aliponyakua ubingwa wa mwaka 2016 nchini Brazil, atatumikia adhabu hiyo hadi Aprili 3, 2025.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako