• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mikoa ya magharibi mwa Tanzania yaimarisha hatua za kuzuia Ebola

    (GMT+08:00) 2019-01-29 09:05:01

    Mikoa ya magharibi mwa Tanzania inayopakana na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kando ya Ziwa Tanganyika imeimarisha hatua za usimamizi na tahadhari kuhusu ugonjwa wa Ebola, kufuatia tahadhari iliyotangazwa na shirika la afya duniani WHO.

    Mganga mkuu wa Mkoa wa Kigoma Bw. Paul Chaote, amesema kwa sasa wameanzisha vituo 14 vya matibabu ya Ebola, na wako kwenye tahadhari ya saa 24 kwa siku.

    Kwa mujibu wa WHO, hadi kufikia tarehe 15 January kulikuwa na maambukizi 663 ya Ugonjwa wa Ebola na vifo 407 nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

    Sudan Kusini ambayo pia inapakana na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ikishirikiana na WHO na wadau wengine wa afya wa kimataifa, jana walianza kutoa chanjo kwa wafanyakazi walioko mstari wa mbele, kwenye kuzuia hatari ya ugonjwa wa Ebola. Waziri wa afya wa nchi hiyo Bw. Riek Gai Kok, amesema hatua hiyo ni sehemu ya juhudi za kuzuia Ebola kutoka nchini DRC.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako