• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania yapoteza dola milioni 145 kila mwaka kutokana na mafuriko na ukame

    (GMT+08:00) 2019-01-29 09:05:24

    Mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kupunguza madhara ya majanga katika kanda ya Afrika Bw. Imjad Abbashar, amesema Tanzania imekuwa ikipoteza takriban dola milioni 145 kwa mwaka kutokana na mafuriko na ukame.

    Akiongea mjini Dodoma kwenye ufunguzi wa warsha ya siku tano kuhusu makadirio ya hatari ya majanga, Bw. Abbashar amesema sekta za nyumba na kilimo ndio zinaathiriwa zaidi mafuriko. Amesema sekta za kilimo na uzalishaji umeme kwa nishati ya maji huwa zinapoteza dola milioni 100 kila mwaka, na asilimia 10 ya watu na mifugo nchini Tanzania, pia huathiriwa na mafuriko.

    Katibu mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Bibi Maimuna Tarishi, pia amesema kati ya mwezi Januari na Desemba mwaka jana, mafuriko yaliathiri wilaya 50, kusababisha vifo 71, na kuwajeruhi watu 64 na kuharibu nyumba kadhaa ikiwa ni pamoja na shule.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako