• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Botswana kuwa mwenyeji wa mazungumzo ya mpaka wa pamoja wa Makubaliano ya Montreal

    (GMT+08:00) 2019-01-29 09:19:40

    Kwa kushirikiana na Shirika la mpango wa maendeleo la Umoja wa Mataifa, Botswana itakuwa mwenyeji wa mazungumzo ya pamoja kuhusu mpaka kwa ajili ya maofisa wa forodha kutoka Botswana, Namibia, Zambia na Zimbabwe kuanzia tarehe 29 hadi 31.

    Taarifa iliyotolewa jana na wizara ya mazingira, maliasili na utalii ya Botswana inasema, mazungumzo hayo ni sehemu ya Makubaliano ya Montreal ya kukabiliana na vitu vinavyoweza kupunguza tabaka ozoni, na lengo lake kuu ni kuhimiza mazungumzo kati ya nchi jirani ili kufanikisha utekelezaji wa makubaliano hayo na kubadilishana habari.

    Botswana ilijiunga na Makubaliano ya Vienna ya kuhifadhi Tabaka Ozoni na Makubaliano ya Montreal kuhusu Vitu vya Kupunguza Tabaka Ozoni mwaka 1992.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako