• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya Nigeria yatetea kusimamishwa kazi kwa jaji mkuu

    (GMT+08:00) 2019-01-29 09:23:44

    Serikali ya Nigeria imetetea uamuzi wa kusimamishwa kazi kwa jaji mkuu kutokana na kukiuka kanuni za kutangaza mali. Waziri wa habari na utamaduni wa Nigeria Bw. Lai Mohammed alisema huko Abuja kuwa kusimamishwa kazi kwa jaji mkuu Bw. Walter Onnoghen, ni matokeo ya ukiukaji wake wa kanuni za maadili kwa maafisa wa umma, na hakuna uhusiano na uchaguzi ujao utakaofanyika mwezi Februari.

    Rais Muhammdu Buhari wa Nigeria alitangaza uamuzi huo Ijumaa wiki iliyopita na kaimu jaji mkuu aliapishwa kushika madaraka siku hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako