• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Zambia bado haijafikia lengo la Umoja wa Mataifa la kupunguza vifo vinavyosababishwa na ajali za barabarani

    (GMT+08:00) 2019-01-29 18:32:32

    Takwimu zilizotolewa kuhusu vifo vilivyosababishwa na ajali za barabarani nchini Zambia mwaka jana zinaonyesha kuwa nchi hiyo bado iko mbali kutimiza lengo la Umoja wa Mataifa la kupunguza vifo hivyo kwa asilimia 50.

    Takwimu zilizotolewa wiki iliyopita na polisi nchini humo zimeonyesha kuwa, nwaka jana, watu 1,817 walifariki katika ajali 30,652 za barabarani nchini Zambia.

    Mwenyekiti wa Mfuko wa Usalama barabarani nchini Zambia Bw. Daniel Mwamba amesema, usalama barabarani na usafiri bora vinapaswa kuwa kipaumbele kwa ajenda za kisiasa kama nchi hiyo inatakiwa kupiga hatua dhahiri katika kutimiza lengo la Umoja wa Mataifa la kupunguza vifo vinavyotokana na ajali za barabarani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako